D Voice Ft Zuchu – Nani LYRICS

D Voice Ft Zuchu – Nani LYRICS -“Wimbo ‘Nani‘ ni ushirikiano kati ya msanii wa Tanzania, D Voice, na Zuchu, ambaye pia ni msanii maarufu kutoka Tanzania. Huu ni wimbo wa mapenzi ambao unazungumzia maswali na mashaka yanayoweza kuibuka katika mahusiano.

Umejaa vionjo vya Afrobeat na Bongo Flava, na sauti za D Voice na Zuchu zinakamilishana vizuri, zikitoa hisia za upendo na ugumu unaohusishwa na kutafuta ukweli katika mapenzi. Maneno ya wimbo huu yana mguso wa kipekee na yamepokelewa vyema na mashabiki wa muziki nchini Tanzania na kwingineko.”

D Voice Ft Zuchu – Nani LYRICS

Aai..Pablo (Mr Lg)
Ai sweetie..
Kuna kitu mi nataka nikuambie..
Lakini naogopa..
Utaniona ka nina wivu hivi..

Oooh sweetie..
Nikunong’oneze wa pembeni wasisikie..
Maana naogopa..
Wataniona ka nina wivu hivi..
Asa sijui ndio ujinga..
Sijui ndo ufala..
Au sijui mazoea..
Ila napata tabu ukiwa mbali maa..
Maana nashindwa..
Kula hata kulala..
Mnyonge nanyong’onyea..
Mwenzio napata tabu ukiwa mbali maa..

PAKUA AUDIO YAKE HAPA: D voice Ft Zuchu – Nani

Honey kwako mi chizi poyoyo
Usiende mbali Nami,
We ndio tulizo la moyo (x2)

Ooh na kama sio wewe (Nani)..
Wa kuniliwaza (Nani)..
Kunibembeleza (Nani)..
Wa kunipepea nilale (Nani)..

Instrumentals…

Mhhhh..
Zuuh Chu chu chu..
Kuna venye husema..
Unaniteka na kuwa chakaram..
Hii inaitwaje kitaalam..
Ukitajwa kimoyo ni paaah..
Why why why why Tam..
Mshwiti Mshwiti bubble gum (bubble gum)..
Yani yam yam yam yam yam..
Ndo mapenzi au ufalaa..
Why why why..
kwanza yote tisa kumi..
Moyo umeuhamisha kambi..
Kanipa penzi sabuni..
Lanitakatisha dhambi..
Wanasubiri livunjike penzi hili..
Hatutishwi na tumbili..
Kuachana apende mwenyezi..
Honey kwako mi chizi poyoyo

Usiende mbali we ndo tulizo la moyo (2x)
Na kama si wewe (Nani)..
wa kuniliwaza (Nani)..
Kunibembeleza (Nani)..

Wa kunipepea nilale (Nani)..
Na kama si wewe (Nani)..
Na kama si weweeeee (Nani)..
Naani Nani
Wa kunidekeza..

Instrumentals..

kamix laizer…

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here